17 Januari 2015 - 11:32
Marekani na Israel zalaani uamuzi wa mahakama ya kimataifa kuichunguza Israel

Israel ilikomesha uchokozi wake kwa nchi ya Lebanon baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanajeshi wa Hizbollah, ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Israel, kipigo hicho kilipelekea majeshi ya Israel kunyoosha mikono na kuomba sulhu katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006.

Marekani imeungana na Israel kulaani uamuzi wa mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu kuanzisha uchunguzi wa awali kuhusu uwezekano kwamba Israel ilitenda uhalifu wa kivita dhidi ya Wapalestina.

Marekani na Israel zimeutaja uamuzi huo ni dhihaka itakayokuwa na matokeo mabaya. Mwendesha mashitaka mkuu wa mahakama hiyo ya ICC Fatou Bensouda amesema hapo jana kuwa ofisi yake itaendesha uchunguzi kamili, huru na usiogemea upande wowote kuhusu madai kuwa Israel ilifanya uhalifu wa kivita dhidi ya Palestina ikiwemo mashambulizi yaliyofanywa katika ukanda wa Gaza mwaka uliopita.Uamuzi huo wa Bensouda unakuja baada ya Palestina kujiunga rasmi na mkataba wa Roma unaounda mahakama hiyo mapema mwezi huu na kuiruhusu kuwasilisha kesi za uhalifu wa kivita dhidi ya Israel. Kiasi ya wapalestina 2,200 na waisrael 73 waliuawa katika vita vya Gaza.

Marekani imekuwa ikiitetea Israel pamoja na kwamba Israel imekuwa ikifanya jinai na mauaji ya kiholela dhidi ya raia madhulumu wa Palestina.

Israel ndio taifa lenye rekodi ya juu ya uchokozi na ukiukaji wa haki za binadamu na kuvunja kanuni za kimataifa kwa kutegemea utetezi inaoupata kutoka kwa serikali ya Marekani.

Israel ilikomesha uchokozi wake kwa nchi ya Lebanon baada ya kupata kipigo kikali kutoka kwa wanajeshi wa Hizbollah, ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya Israel, kipigo hicho kilipelekea majeshi ya Israel kunyoosha mikono na kuomba sulhu katika vita vya siku 33 vya mwaka 2006.

Kikosi cha jeshi cha Hizbollah ni kikosi cha waislamu wa dhehebu la Shia ithna asharia kinachopata mafunzo na udhamini kutoka kwa jamhuri ya kiislamu ya Iran.

Tags